Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kubugia dawa jambo ambalo ni hatari sana. Kupungua nguvu za kiume si ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Jambo hili imekuwa nilikueleza mara Kwa mara sana katika video zangu, na sehemu mbalimbali za makala zangu, hasa katika makala kuu: Matibabu Sahihi ya Nguvu za Kiume nimelifafanua kwa mapana na marefu zaidi.
Ndugu msomaji unapopungukiwa nguvu za kiume maana yake kuna vitu ndani ya mwili wako havifanyi kazi vizuri. Na ndani ya mwili kuna vitu zaidi ya 100 vinavyofanya kazi ya nguvu za kiume, mathalani kuna moyo, kuna figo na kofia zake, kuna tezi mbalimbali ziko zaidi ya 10, kuna misuli tofauti tofauti zaidi ya kumi, kuna mishipa ya neva tofauti tofauti zaidi ya 20, kuna homoni zipo zaidi ya 10. Kuna vitu vingi sana. Orodha ni ndefu.
Sasa unapopungukiwa nguvu za kiume maana yake ni kwamba kuna vitu au viungo kadhaa mwilini havifanyi kazi zake vizuri ipasavyo; aidha inaweza kuwa tezi fulani au misuli fulani au homoni fulani na kadha wakadhaa. Na Kuna sababu zinazopeleka vitu hivyo kushindwa kufanya kazi yake vizuri ikiwemo maradhi, tabia na mtindo wa maisha. Mathalani, ugonjwa wa kisukari unaweza kuharibu kabisa mishipa ya neva na homoni kadhaa na hivyo kusababisha upungigu wa nguvu za kiume. Au tabia ya kujichua inaathiri vitu zaidi ya 18 mwilini vinavyohusika na nguvu za kiume ikiwemo mishipa muhimu sana ya parasympathetic nerves ambayo kazi yake kuu ni kusimamisha uume na kufungua milango ya shahawa, ndiyo maana waliojichua wengi hufika kileleni haraka sana, au ulaji mbaya - kuna vyakula zaidi ya 50 vinavyoua nguvu za kiume moja kwa moja.
Sasa daktari anayekutibu upungufu wa nguvu za kiume anatakiwa awe daktari mtaalam aliyebobea katika uzazi wa mwanaume na afya ya mfumo wa mkojo. Na pia awe na dawa sahihi za asili zinazoenda kwenye chanzo cha tatizo.
Sasa leo kosa wanalofanya wanaume wengi ni kukurupuka kubugia dawa pale tu wanapokabiliwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume. Akisikia dawa inatakangazwa ya nguvu za kiume anakimbilia kutumia. Hilo ni kosa kubwa sana. Hakuna dawa moja inayotibu kila mgonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume. Kila mwanaume ana dawa yake kulingana na tatizo lake.
Utakuta mtu anatangaza dawa moja ya nguvu za kiume ati dawa hiyo ina uwezo wa kutibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wagonjwa wote. Hilo ni kosa kubwa sana.
Kuna mtu kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu tezidume haifanyi kazi vizuri mwingine kwa sababu homoni ya testestoroni iko chini, mwingine kwa sababu moyo hausukumi damu vizuri, je wote utawapa dawa aina moja? Nguvu za kiume hazitibiwi hivyo kabisa. Kwa matibabu ya mtindo utahangaika dunia nzima na utatumia pesa nyingi sana hautapona kabisa. Utaharibu pesa zako bure na muda wako bure lakini hamna kitu, na kibaya zaidi unaweza hata kushangaa tatizo ndiyo linaongezeka zaidi. Hata chakula huwezi kuwashauri wagonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume chakula cha aina moja. Kila mwanaume atashauriwa chakula chake kulingana na tatizo lake, chanzo chake, sababu zake na ukubwa wa tatizo. Mathalani, kuna mgonjwa unaweza kumshauri atumie ndizi na mwingine ukamshauri kitu kingine kabisa.