TIBA HAZIANZI KWA DHANA—HUANZA KWA UCHUNGUZI
Katika tiba za kisasa, hakuna daktari anayeanza kutibu kukosa hamu ya mapenzi kwa kubahatisha. Kila kitu huanzia kwenye diagnosis ya kitaalamu (clinical evaluation).
Mashirika ya afya kama American Urological Association na European Association of Urology yanasisitiza kwamba tatizo la libido ya chini linapaswa kuchunguzwa kwa kina kabla ya matibabu yoyote kuanza.
Kwa lugha rahisi:
huwezi kutibu bila kujua chanzo. Ni kama kutengeneza gari bila kujua limeharibika wapi.
1. UCHUNGUZI WA AWALI (CLINICAL ASSESSMENT)
Tunaanza kwa mahojiano ya kina yanayoitwa medical history taking.
Hii hatua ni muhimu sana kwa sababu takribani 40–60% ya kesi za low libido zinahusiana na psychological factors, kulingana na tafiti za The Journal of Sexual Medicine.
2. VIPIMO VYA MAABARA (LABORATORY TESTS)
Baada ya historia, tunaweza kukushauri kufanya vipimo vya damu kama:
(a) Testosterone Total & Free
(b) Prolactin Test
(c) Blood Sugar (Glucose / HbA1c)
(d) Thyroid Function Tests
Tezi ya thyroid ikiwa haifanyi kazi vizuri:
- Libido hushuka
- Mood hubadilika
- Energy hupungua
3. TATHMINI YA AFYA YA AKILI (MENTAL HEALTH EVALUATION)
Afya ya akili ina nafasi kubwa sana. Hapa tunaangalia
- Depression
- Anxiety
- Chronic stress
Kulingana na World Health Organization, afya ya akili ni sehemu muhimu ya afya ya uzazi na haipaswi kutenganishwa.
4. UCHUNGUZI WA MTINDO WA MAISHA (LIFESTYLE REVIEW)
Hapa tunaangalia angalia:
- Usingizi (sleep quality)
- Mazoezi
- Lishe
- Uzito (BMI)
- Pombe na sigara
Mfano rahisi wa kisayansi:
> mtu anayekula vizuri + analala vizuri + anafanya mazoezi = ana testosterone bora zaidi.
5. MATIBABU YA KISAYANSI (EVIDENCE-BASED TREATMENT)
Baada ya chanzo kubainika, matibabu hufuata moja au mchanganyiko wa njia hizi:
5.1 Kurekebisha mifumo ya kihomoni itakavyobainika tutakupa dawa maalumu za Kuongeza kulingana na tatizo chanzo chake. Dawa zetu za kutibu hisia za mapenzi:
- Huongeza libido
- Huongeza energy
- Huboresha mood
5.2 Psychological Therapy
Pia tutakupa ushauri na dawa za kuondoa:
- Stress
- Anxiety
- Depression
5.3 Matibabu ya Magonjwa ya Msingi
- Kisukari → kudhibiti sukari
- Presha → kudhibiti shinikizo la damu
- Thyroid disorders → kurekebisha homoni n.k
5.4 Lifestyle Modification (MSINGI WA TIBA YA KISASA)
Hapa tunaweza kukushauri vitu vingi ikiwa ni pamoja na:
Mazoezi (angalau dakika 150 kwa wiki)
Usingizi wa saa 7–9
Lishe yenye protini na mafuta mazuri
Kupunguza au kuacha kabisa pombe na sigara n.k
MUHTASARI
Matibabu ya kukosa hamu ya mapenzi si dawa moja tu. Ni mchakato wa:
1. Uchunguzi wa kitaalamu
2. Vipimo vya homoni na afya ya mwili
3. Tathmini ya akili
4. Mabadiliko ya maisha
5. Matibabu maalum kulingana na chanzo